Deutsche Welle ni Shirika la Kimataifa la Utangazaji la Ujerumani, linaloandaa vipindi vya Televisheni, Radio na Mtandao wa Intaneti kwa ajili yako katika lugha 30 - popote ulipo ulimwenguni.

Tafadhali tusaidie kuyafanya majadiliano katika kituo hiki kuwa safi na ya kukubalika na jiepushe kutumia lugha ya kibaguzi au uchafu pamoja na matusi ya kibinafsi.

Kwa taarifa zaidi tafadhali bonyeza link ya "DW Netiquette" hapo chini.
Tunakusihi ushiriki katika utafiti wetu wa mtandaoni ili tupate maoni yako. Bonyeza kiunganishi kwa maelekezo zaidi: surveys.dw.com/c/vcemmsxp
www.dw.com/en/dws-netiquette-policy/a-5300954


DW Kiswahili

Rafiki yako wa karibu anakutumia meseji:

"Nitumie laki 2 leo, nitakurudishia mwisho wa mwezi."

Unafanya nini?

3 weeks ago | [YT] | 34

DW Kiswahili

Kukopeshana kati ya marafiki kunajenga au kunaharibu urafiki? Kwa nini baadhi ya marafiki hupotea baada ya kukopeshwa? Je, ni bora kukopa benki, SACCO au kwa rafiki? Kuna sheria gani zisizoandikwa ambazo kila kijana anapaswa kujua kabla ya kumkopesha mtu? Kwenye #KurunziLive leo tunafungua mjadala ambao vijana wengi huukwepa lakini kila siku wanauishi.
Tuambie mapema. Andika maoni yako kabla ya kipindi. Maoni yako yanaweza kujadiliwa LIVE. #DWKiswahili #KurunziLive https://www.youtube.com/watch?v=Cc6zs...

3 weeks ago (edited) | [YT] | 19

DW Kiswahili

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema mlipuko wa Ebola nchini DR Congo umeenea hadi mikoa sita, huku mahitaji ya vitanda vya matibabu na wahudumu wa afya yakiendelea kuongezeka. Tayari zaidi ya watu 3,175 wamefariki na zaidi ya visa 6,000 vimerekodiwa. Vituo vya matibabu vinaongezwa, lakini changamoto bado ni kubwa #DWKiswahili #AfyaYako #ebola #Mripukowaebola #ebolavirus

1 month ago | [YT] | 1

DW Kiswahili

Wapiga kura katika jimbo la Saxony-Anhalt wanachagua bunge jipya katika uchaguzi unaoweza kubadili mwelekeo wa siasa za Ujerumani.
Chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD kinaongoza kwa mbali katika kura za maoni dhidi ya CDU cha Kansela Friedrich Merz. Ikipata wingi wa moja kwa moja, AfD inaweza kuwa chama cha kwanza cha mrengo mkali wa kulia kuongoza jimbo la Ujerumani tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia.
Ikikosa wingi huo, hesabu za kuunda serikali zinaweza kuilazimisha CDU kutegemea vyama ambavyo imekuwa ikikataa kushirikiana navyo. Hali hiyo itauweka kwenye majaribu “ukuta wa kisiasa” unaotumiwa kuitenga AfD na inaweza kuongeza shinikizo kwa Kansela Merz.
Je, uchaguzi wa Saxony-Anhalt utakuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa katika siasa za Ujerumani?
Fuatilia matokeo na uchambuzi wetu kupitia DW Kiswahili.
#SaxonyAnhalt #Ujerumani #AfD #CDU #Uchaguzi

1 month ago | [YT] | 11

DW Kiswahili

Hii ndio taswira ya mchora katuni wetu Said Michael kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Tanzania iliyoanza jana, ikiwa ni ziara yake ya pili mwaka 2026 yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara kati ya mataifa hayo mawili, wakati ambapo serikali zote mbili zimekuwa zikikabiliwa na shutuma za kukandamiza demokrasia.

2 months ago | [YT] | 81

DW Kiswahili

Dunia inaadhimisha siku ya Kimataifa ya Mandela (Julai 18). Kaulimbiu ya mwaka huu “Bado iko mikononi mwetu kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa,” inaangazia wajibu unaoendelea wa kuinua na kuimarisha jamii. Katuni inamulika mchango wa hayati Nelson Mandela katika jamii, mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na kuunganisha jamii nzima. Je wewe unaitizama vipi Siku ya Mandela Duniani, umuhimu wa siku yenyewe ukilinganisha na hali halisi ya sasa nchini Afrika Kusini? @wakudata #DWKiswahili

3 months ago | [YT] | 30

DW Kiswahili

Kocha wa Misri Hossam Hassan ameeleza kuwa timu yake haikutendewa haki na kwamba maamuzi ya marefarii yalikuwa ya upande mmoja. Amedai kuwa matokeo hayo yalitokana na "dhuluma ya wazi" na hata kutangaza kuwa hatotazama tena mechi zilizosalia za Kombe la Dunia. Je, unadhani kuna upendeleo kwa baadhi ya timu au wachezaji kwenye michuano hiyo?

3 months ago | [YT] | 38

DW Kiswahili

Taswira ya Siku ya Bahari Duniani, inayoadhimishwa kila Juni 8. Kibonzo kinaangazia dhana potofu ya utupaji taka baharini na athari zake kwa maisha ya viumbe wa majini

4 months ago | [YT] | 41

DW Kiswahili

MJADALA ⚽: Timu 10 za Afrika zinashiriki kwenye Kombe la Dunia 2026!
Kuanzia DR Kongo hadi Ghana, je, nani atavuka hatua ya makundi?
Ukiangalia wapinzani wa timu za Afrika, je, kuna nafasi ya historia mpya 2026? Miaka 50 baadaye, Leopards wanarudi jukwaani. Je, wataweza kushindana na vigogo? Afrika Kusini yafungua dimba dhidi ya Mexico. Lakini makundi ni magumu—nani ataibuka mshindi? Usikose kutegea sikio mjadala huu. #DWKiswahili

4 months ago | [YT] | 32

DW Kiswahili

Je, unajua kuwa unene uliopitiliza ni miongoni mwa sababu kuu za vifo vinavyoweza kuzuilika? Tatizo hili limekuwa kimya lakini hatari, na linaendelea kuathiri watu wa rika zote. Mjadala huu unalenga kufungua macho yetu kuhusu Obesity, kwa kuelezea chanzo chake, athari zake na namna ya kuchukua hatua mapema. Lakini je unadhani unene uliopitiliza ni kosa la mtu binafsi au ni tatizo linalosababishwa na mfumo wa maisha wa leo? Tuambie maoni yako #dwkiswahili https://www.youtube.com/watch?v=cobH8...

6 months ago | [YT] | 42