DODOMA RS TV CHANNEL



DODOMA RS TV CHANNEL

Live: UZINDUZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA

4 days ago | [YT] | 0

DODOMA RS TV CHANNEL

AFYA NI MTAJI. JIKINGE KWA BIMA YA AFYA.

1 week ago | [YT] | 0

DODOMA RS TV CHANNEL

WANANCHI 111,515 DODOMA KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KUPITIA UFADHILI WA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu
DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma unatarajia kuzindua rasmi mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Alhamisi, Oktoba 22, 2026, katika Viwanja vya Machinga Complex jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema wananchi 111,515 wananufaika kupitia ufadhili wa Serikali, huku akiwahimiza wananchi kujiunga na bima ya afya ili kulinda afya, kipato na akiba za familia.

Katika uzinduzi huo, wananchi watapata huduma mbalimbali za uchunguzi wa afya bila malipo, elimu kuhusu bima ya afya na fursa ya kusajili kaya zisizo na uwezo zinazostahili kunufaika na mpango huo.

Mhe. Senyamule amewakaribisha wananchi wa Dodoma na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kunufaika na huduma hizo.

AFYA NI MTAJI. JIKINGE KWA BIMA YA AFYA!


#DodomaYaMafanikio #AfyaNiMtaji #BimaYaAfyaKwaWote #SerikaliKazini
#KaziInaendelea
#NHIF

1 week ago | [YT] | 2

DODOMA RS TV CHANNEL

111,515 DODOMA RESIDENTS TO BENEFIT FROM GOVERNMENT-FUNDED HEALTH INSURANCE

By Our Correspondent
DODOMA RS

Dodoma Region is set to officially launch the Universal Health Insurance Scheme on Thursday, October 22, 2026, at Machinga Complex Grounds in Dodoma City.

Dodoma Regional Commissioner, Hon. Rosemary Senyamule, has announced that 111,515 residents are benefiting from Government-funded health insurance, while urging citizens to enrol in health insurance schemes to protect their health, income, and family savings.

During the launch, residents will access various free health screening services, receive education on health insurance, and have an opportunity to register eligible low-income households for support under the scheme.

Hon. Senyamule has invited residents of Dodoma and neighbouring areas to turn out in large numbers and take advantage of the services.

HEALTH IS WEALTH. PROTECT YOURSELF WITH HEALTH INSURANCE!


#DodomaOfSuccess #HealthIsWealth #UniversalHealthInsurance
#GovernmentAtWork #TheWorkContinues #NHIF

1 week ago | [YT] | 0

DODOMA RS TV CHANNEL

TANZANIA STRENGTHENS PREPAREDNESS AGAINST DISEASE OUTBREAKS

By Our Correspondent
DODOMA RS

Tanzania has assessed the capacity of its health emergency response systems through a Functional Simulation Exercise conducted on October 15, 2026, aimed at strengthening preparedness for outbreaks of infectious diseases, including Ebola.

Speaking during the exercise, the Guest of Honour, Director of the Emergency and Disaster Department at the Ministry of Health, Dr. Erasto Sylvanus, emphasized the importance of strengthening coordination, leadership, and rapid response across all levels of the health system.

The exercise involved Public Health Emergency Operations Centres (PHEOCs) at the national level and in Dodoma, Dar es Salaam, and Arusha regions. It aimed to identify gaps and improve preparedness and response mechanisms for public health emergencies.

This initiative is part of the Government’s efforts to protect public health and safety by strengthening surveillance, coordination, and rapid response systems to disease outbreaks.

2 weeks ago | [YT] | 1

DODOMA RS TV CHANNEL

TANZANIA YAIMARISHA UTAYARI DHIDI YA MAGONJWA YA MLIPUKO

Na Mwandishi Wetu
DODOMA RS

Tanzania imepima uwezo wa mifumo ya dharura za afya kupitia zoezi la majaribio ya utendaji (Functional Simulation Exercise) lililofanyika Oktoba 15, 2026, kwa lengo la kuimarisha utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, ikiwemo Ebola.

Akizungumza katika zoezi hilo, Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Dharura na Maafa katika Wizara ya Afya, Dkt. Erasto Sylvanus, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uratibu, uongozi na mwitikio wa haraka katika ngazi zote za mfumo wa afya.

Zoezi hilo limehusisha vituo vya Operesheni za Dharura za Afya ya Umma (PHEOC) vya ngazi ya Taifa na mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Arusha, likilenga kubaini mapungufu na kuboresha mifumo ya maandalizi na kukabiliana na dharura za kiafya.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Serikali za kulinda afya na usalama wa wananchi kupitia mifumo imara ya ufuatiliaji, uratibu na mwitikio wa haraka dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

2 weeks ago (edited) | [YT] | 0

DODOMA RS TV CHANNEL

RC SENYAMULE AKAGUA MAANDALIZI YA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE, ASISITIZA UKAMILISHAJI WA MIUNDOMBINU

Na Mwandishi Wetu – Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, leo Julai 8, 2026, ametembelea na kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Nanenane vya John Samwel Malecela Nzuguni, Jijini Dodoma.

Baada ya ukaguzi huo, Mhe. Senyamule amewataka wasimamizi wa maandalizi kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati miundombinu yote muhimu, hususan lango kuu la kuingilia, ili viwanja hivyo viwe katika hali nzuri na viwe tayari kupokea washiriki na wageni watakaohudhuria maonesho hayo.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuboresha na kukamilisha huduma zote za kijamii, ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, umeme wa uhakika, vyoo vya kutosha, usafi wa mazingira pamoja na huduma nyingine muhimu, ili kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi na wadau watakaoshiriki Maonesho hayo.

"Maandalizi mazuri yataongeza hadhi ya Maonesho ya Nanenane na kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Kilimo kuonesha teknolojia, ubunifu na mafanikio yanayochochea maendeleo ya uchumi na kuimarisha usalama wa chakula," amesema Mhe. Senyamule.

Ameongeza kuwa maandalizi ya mapema na ushirikiano wa wadau wote ni msingi wa kufanikisha Maonesho ya Nanenane, ambayo yanalenga kuonesha mafanikio, ubunifu na teknolojia mbalimbali katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, sambamba na kuwakutanisha wadau kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujenga fursa za maendeleo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ugani, Wizara ya Kilimo, Bi. Upendo Mndeme, amesema maandalizi yote yanatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 16, 2026. Ameeleza kuwa maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa yatafanyiwa kazi kwa wakati ili kuhakikisha viwanja vinakuwa tayari kwa ajili ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) mwaka huu.



#DodomaFahariYaWatanzania
#KeroYakoWajibuWanguTabasamuNaSamia
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#Nanenane2026

3 months ago | [YT] | 3