Furaha ya familia iligeuka kuwa msiba baada ya watoto wao wanne watano kufariki saa 24 tu baada ya kuzaliwa. - Madaktari wanasema sababu zilikuwa mchanganyiko wa matatizo ikiwa ni pamoja na kuzaliwa kabla ya wakati, chini ya miezi 6, uzito mdogo sana na kukosa kuumbika kamili viungo vya mwili. - Mimba nyingi hubeba hatari kubwa ya kuzaliwa kabla ya wakati na matatizo makubwa, na kufanya utunzaji kuwa mgumu hata kwa huduma maalum ya watoto wachanga na vifaa vya kuwatunzia.
Francesca Albanese, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu, ameonya kwamba hatu ay aIsrael kuondoa vifusi kwa katika Gaza ya Palestina kunaweza kuharibu ushahidi muhimu wa "uhalifu wa kikatili" na kuzuia kupatikana tena kwa mabaki ya binadamu.
"Athari zake ni kubwa. Vifusi vya Gaza vina mabaki ya binadamu na ushahidi wa kimwili unaohusiana na uchunguzi wa madai ya uhalifu wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari," Albanese alisema mnamo Septemba 7.
Alitaka kupatikana na kutambuliwa kwa mabaki ya binadamu, na unakili wa kimfumo na uhifadhi wa ushahidi unaowezekana kabla ya vifusi kuhamishwa au kupondwa, huku Wapalestina wakiongoza mipango ya kuondoa vifusi na wachunguzi wa jinai wa kimataifa wakisimamia mchakato huo.
Pia alionya mataifa na makampuni yanayohusika katika uondoaji kwamba kuharibu ushahidi wa uhalifu wa kimataifa kunaweza kuwaweka katika mashtaka ya jinai ya kimataifa. "Kuharibu ushahidi wa uhalifu wa kikatili ni kinyume cha sheria," alisisitiza.
Makadirio ya idadi ya watu ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa idadi ya watu duniani ilifikia bilioni 8.23 katikati ya mwaka 2025, ikiendelea na mwelekeo wake wa kupanda kwa miongo kadhaa.
India inasalia kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani, ikifuatiwa na China na Marekani, huku mataifa hayo matatu yakichangia karibu 39.2% ya idadi ya watu duniani.
Makadirio ya hivi karibuni pia yanaangazia mabadiliko ya mitindo ya idadi ya watu, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa viwango vya uzazi, umri mrefu wa kuishi, na idadi ya watu kuzeeka duniani kote.
Kwa miaka kadhaa Uturuki imetoa mchango mkubwa kwa operesheni za vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa kote barani Afrika, kusaidia kuleta usalama katika nchi hizo.
Haya ni baadhi ya maeneo ambapo vikosi vya Uturuki vimehudumu katika mpango wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.
FIFA yamuondoa mwamuzi Msomali
Artan katika Kombe la Dunia baada
ya kuzuiwa kuingia Marekani.
FIFA imesema haina uwezo wa kushawishi uamuzi wa Marekani kumruhusu Omar Artan, na kusema kuwa uamuzi huo unabaki kwa Marekani ambayo ni nchi mwenyeji.
Mwamuzi huyo wa Somalia Omar Artan aliyewahi kupata tuzo ameondolewa katika orodha ya waamuzi waliotakiwa kuwepo katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuzuiwa kuingia Marekani, FIFA imesema Jumatatu.
Msemaji wa FIFA amethibitisha katika taarifa kwamba, Artan, ambae alikataliwa kuingia nchini Marekani baada ya kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami Jumamosi, hatakuwa na jukumu lolote katika michuano ya Kombe la Dunia.
Iwapo angekubaliwa kuingia nchini Marekani, Artan angekuwa raia wa kwanza wa Somalia kuwa mwamuzi katika Kombe la Dunia.
Watu kutoka nchi 36, wakibaini mfumo wa wazi: Imani kwa Benjamin Netanyahu ni ndogo na mtazamo wa dunia kuhusu Israel ni hasi zaidi.
Wastani wa asilimia 67 hawaipendi Israel, ilhali asilimia 25 wakiwa wanalipenda taifa hilo.
Katika nchi nyingi ambapo watu wamehojiwa, wengi wanasema hawana imani kuwa Netanyahu atafanya jambo sahihi katika masuala ya dunia, ikiashiria mtazamo wa dunia ambao umeangazia matukio ya miezi ya hivi karibuni ya vita vya Israel huko Gaza na kuongezeka kwa vurugu katika kanda, ikiwemo mashambulizi dhidi ya Iran.
COP31 itafanyika mjini Antalya nchini Uturuki mwezi Novemba mwaka huu wakati taifa likijiandaa kwa kongamano kubwa zaidi duniani la tabianchi. Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa utaangazia kuimarisha juhudi kwa tatizo la tabianchi, kutoka kupungiuza hewa chafu hadi kuwa na uchumi endelevu zaidi.
Zaidi ya kuwa mwenyeji, kwa muda mrefu Uturuki imejiweka kama kiongozi maendeleo endelevu duniani na sera ya tabianchi. Moja ya mifano muhimu ni Mradi wa Taka Sifuri, ulioanzishwa 2017 chini ya mlezi wake Mke wa Rais Emine Erdogan, na wenye lengo kupunguza taka kutoka kwenye vyanzo vyake, kuimarisha kasi ya uchakataji, na kuhamasisha utaratibu wa matumizi endelevu.
Tangu kuanzishwa kwake, mradi huo umepanua uchakataji na mifumo ya matumizi ya taka kote nchini, kusaidia kukusanya taka katika majaa na kuchakata ili kupata matumizi yake tena, wakati ukipunguza matumizi ya maji, nishati, na malighafi.
TRT Afrika Swahili
Furaha ya familia iligeuka kuwa msiba baada ya watoto wao wanne watano kufariki saa 24 tu baada ya kuzaliwa.
- Madaktari wanasema sababu zilikuwa mchanganyiko wa matatizo ikiwa ni pamoja na kuzaliwa kabla ya wakati, chini ya miezi 6, uzito mdogo sana na kukosa kuumbika kamili viungo vya mwili.
- Mimba nyingi hubeba hatari kubwa ya kuzaliwa kabla ya wakati na matatizo makubwa, na kufanya utunzaji kuwa mgumu hata kwa huduma maalum ya watoto wachanga na vifaa vya kuwatunzia.
trt
2 weeks ago | [YT] | 5
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Ni nini kimemtokea Emmamuel Nchimbi?
https://youtu.be/75i5o6etyMQ
2 weeks ago | [YT] | 3
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Francesca Albanese, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu, ameonya kwamba hatu ay aIsrael kuondoa vifusi kwa katika Gaza ya Palestina kunaweza kuharibu ushahidi muhimu wa "uhalifu wa kikatili" na kuzuia kupatikana tena kwa mabaki ya binadamu.
"Athari zake ni kubwa. Vifusi vya Gaza vina mabaki ya binadamu na ushahidi wa kimwili unaohusiana na uchunguzi wa madai ya uhalifu wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari," Albanese alisema mnamo Septemba 7.
Alitaka kupatikana na kutambuliwa kwa mabaki ya binadamu, na unakili wa kimfumo na uhifadhi wa ushahidi unaowezekana kabla ya vifusi kuhamishwa au kupondwa, huku Wapalestina wakiongoza mipango ya kuondoa vifusi na wachunguzi wa jinai wa kimataifa wakisimamia mchakato huo.
Pia alionya mataifa na makampuni yanayohusika katika uondoaji kwamba kuharibu ushahidi wa uhalifu wa kimataifa kunaweza kuwaweka katika mashtaka ya jinai ya kimataifa. "Kuharibu ushahidi wa uhalifu wa kikatili ni kinyume cha sheria," alisisitiza.
2 weeks ago | [YT] | 2
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Makadirio ya idadi ya watu ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa idadi ya watu duniani ilifikia bilioni 8.23 katikati ya mwaka 2025, ikiendelea na mwelekeo wake wa kupanda kwa miongo kadhaa.
India inasalia kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani, ikifuatiwa na China na Marekani, huku mataifa hayo matatu yakichangia karibu 39.2% ya idadi ya watu duniani.
Makadirio ya hivi karibuni pia yanaangazia mabadiliko ya mitindo ya idadi ya watu, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa viwango vya uzazi, umri mrefu wa kuishi, na idadi ya watu kuzeeka duniani kote.
2 months ago | [YT] | 6
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Kwa miaka kadhaa Uturuki imetoa mchango mkubwa kwa operesheni za vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa kote barani Afrika, kusaidia kuleta usalama katika nchi hizo.
Haya ni baadhi ya maeneo ambapo vikosi vya Uturuki vimehudumu katika mpango wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.
2 months ago | [YT] | 2
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Kote barani Ulaya, joto linazidi kila sehemu.
Watu wasiopungua milioni 94 wanatarajiwa kukabiliana na hali ya nyuzijoto zaidi ya 35 wiki hii, hasa nchini Ufaransa na Hispania.
Hiki ndicho unachotakiwa kufanya ili usitatizike katika mazingira ya joto.
3 months ago | [YT] | 2
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
FIFA yamuondoa mwamuzi Msomali Artan katika Kombe la Dunia baada ya kuzuiwa kuingia Marekani.
FIFA imesema haina uwezo wa kushawishi uamuzi wa Marekani kumruhusu Omar Artan, na kusema kuwa uamuzi huo unabaki kwa Marekani ambayo ni nchi mwenyeji.
Mwamuzi huyo wa Somalia Omar Artan aliyewahi kupata tuzo ameondolewa katika orodha ya waamuzi waliotakiwa kuwepo katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuzuiwa kuingia Marekani, FIFA imesema Jumatatu.
Msemaji wa FIFA amethibitisha katika taarifa kwamba, Artan, ambae alikataliwa kuingia nchini Marekani baada ya kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami Jumamosi, hatakuwa na jukumu lolote katika michuano ya Kombe la Dunia.
Iwapo angekubaliwa kuingia nchini Marekani, Artan angekuwa raia wa kwanza wa Somalia kuwa mwamuzi katika Kombe la Dunia.
3 months ago | [YT] | 29
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Watu kutoka nchi 36, wakibaini mfumo wa wazi: Imani kwa Benjamin Netanyahu ni ndogo na mtazamo wa dunia kuhusu Israel ni hasi zaidi.
Wastani wa asilimia 67 hawaipendi Israel, ilhali asilimia 25 wakiwa wanalipenda taifa hilo.
Katika nchi nyingi ambapo watu wamehojiwa, wengi wanasema hawana imani kuwa Netanyahu atafanya jambo sahihi katika masuala ya dunia, ikiashiria mtazamo wa dunia ambao umeangazia matukio ya miezi ya hivi karibuni ya vita vya Israel huko Gaza na kuongezeka kwa vurugu katika kanda, ikiwemo mashambulizi dhidi ya Iran.
3 months ago | [YT] | 8
View 1 reply
TRT Afrika Swahili
COP31 itafanyika mjini Antalya nchini Uturuki mwezi Novemba mwaka huu wakati taifa likijiandaa kwa kongamano kubwa zaidi duniani la tabianchi. Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa utaangazia kuimarisha juhudi kwa tatizo la tabianchi, kutoka kupungiuza hewa chafu hadi kuwa na uchumi endelevu zaidi.
Zaidi ya kuwa mwenyeji, kwa muda mrefu Uturuki imejiweka kama kiongozi maendeleo endelevu duniani na sera ya tabianchi. Moja ya mifano muhimu ni Mradi wa Taka Sifuri, ulioanzishwa 2017 chini ya mlezi wake Mke wa Rais Emine Erdogan, na wenye lengo kupunguza taka kutoka kwenye vyanzo vyake, kuimarisha kasi ya uchakataji, na kuhamasisha utaratibu wa matumizi endelevu.
Tangu kuanzishwa kwake, mradi huo umepanua uchakataji na mifumo ya matumizi ya taka kote nchini, kusaidia kukusanya taka katika majaa na kuchakata ili kupata matumizi yake tena, wakati ukipunguza matumizi ya maji, nishati, na malighafi.
3 months ago | [YT] | 5
View 0 replies
TRT Afrika Swahili
Je, Arteta atatemetesha tena uwanjani Jumamosi Mei 30 wakiwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG?
4 months ago | [YT] | 2
View 0 replies
Load more