Mtanzania Halisi we are dealing with providing all kind of news and broadcasting around East Africa.
Pata habari kwa haraka na uhakika kila wakati katika ukurasa huu. USISAHAU KU-SUBCRIBE


MTANZANIA HALISI

TUME YA MADINI RUKWA YATOA ELIMU YA UCHIMBAJI SALAMA NA FURSA ZA UWEKEZAJI LAELA

Ofisi ya madini mkoani Rukwa leo tarehe 8/9/2026 imetoa elimu ya uchimbaji salama afya, utunzaji wa mazingira na ulipaji wa kodi za serikali, pamoja na furusa uwekezaji katika sekta ya madini zinazo patikana katika mji mdogo wa Laela.

Mkutono huo uliuzuliwa na wachimbaji wa dogo wa madini ujenzi (Mchanga, Komoto, mawe, vifusi), wafanyabiashara wa tofali za kuchoma, wasafirishaji wa madini Ujenzi, wananchi pamoja na viongozi wa serikali za mitaa (Diwani, watendaji) pamoja na mwenyekiti wa mtaa wa laela kwa ajili ya kuwapa uwelewa wa pamoja juu ya aina za madini na njia ya uchimabji salama.

Aidha, wadau wote walioshiriki walipewa nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa hapo ,na kuwa na uelewa wa pamoja ulipaji wa kodi za Serikali ya madini wanayochimba au kuchoma tofali. Pia wadau wote walielimishwa kuhakikisha wanalipa Kodi za madini ujenzi kwa mjibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 sura ya 123 na malekebisho yake yanayoendelea kuboreshwa.

Elimu hiyo imetolewa na maafisa kutoka ofisi ya madini Mkazi Rukwa ambao ni Mjiolojia Leonidas kairu, afisa mazingira Mnubi Edwin Neke, Bw. Alfakisadi Martine (msimamizi wa Kituo cha Laela) Na Richard Mshimata (Dereva).

Mada kuu katika mkutano huo ni pamoja na ulipaji wa tozo za serikali zitokanazo na madini ujenzi kama vile kokoto, mchanga, vifusi vya udogo , tofali za kuchoma pamoja na moramu.
Kingine ni utunzji wa mazingira na fursa anazoweza kupata mchimbaji kupitia kumiliki leseni ndogo (PML).

1 month ago | [YT] | 8

MTANZANIA HALISI

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Ushirikiano kati Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuongeza uwekezaji na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Maji katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2024 hadi 2025.

Waziri Aweso amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi, sambamba na kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma za maji nchini.

Amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ya maji vijijini, kwasababu Serikali inalenga kumaliza uhaba wa maji katika vijiji 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya huduma ya maji.

Waziri Aweso amesisitiza matumizi bora ya fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kuzielekeza katika maeneo yenye mahitaji makubwa, na kutaka utekelezaji wa miradi uzingatie thamani ya fedha kwa kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya wananchi.

2 months ago | [YT] | 10

MTANZANIA HALISI

https://youtu.be/8KRpq8QBL-s

MAPYA YAIBUKA KESI YA MUSIBA NA MEMBE WAKILI AFUGUKA MAZITO

6 months ago | [YT] | 8

MTANZANIA HALISI

https://youtu.be/xWP8-2weZvU

MAISHA YA INSTAGRAM

8 months ago | [YT] | 1

MTANZANIA HALISI

https://youtu.be/W__j86rk3yo

Sekeseke la HAule wa Jeraha Usisahau Kusubscribe

10 months ago | [YT] | 1

MTANZANIA HALISI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiombewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

11 months ago | [YT] | 7