Focus News Tanzania Tv 1, ni channel yako ya TV ya kiganjani ambapo utapata habari mbalimbali ikiwemo habari za kijamii, Siasa, Michezo na Burudani bila kusahau mahojiano katika mada mbalimbali.
Tupo Dodoma Makao Makuu ya Tanzania maeneo ya Ipagala jirani na kanisa la kwa Evance. Jiunge nasi kwa kubonyeza mandishi mekundu yaliyoandikwa Subscribe na kisha bonyeza alama ya kengere na hapo utakuwa umeungana nasi mubashara.
Akhsante kwa kuendelea kuichagua Focus News Tanzania kuwa channel yako pendwa ya TV ya kiganjani.
Focus News Tanzania Tv 1,
Mobile:.+255755834996
Whatsapp:β¦.+255755834996
E-mail:...focusnewsroomtanzania@gmail.com
Focus News Tanzania Tv 1
WAOUTH WAFANYA SHAMBULIO JIPYA UWANJA WA NDEGE SAUDI ARABIA
Mtu mmoja ameuawa na karibu watu kumi na wawili kujeruhiwa katika shambulio jipya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh siku ya Jumapili, mamlaka ya Saudi Arabia iliripoti.
Shambulizi hili linakuja siku moja baada ya shambulio lingine lililodaiwa kutekelezwa na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen ambalo liliua watu 13 na kujeruhi zaidi ya 300.
Vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Saudi Arabia huko Yemen vilisema kombora lisilojulikana lililenga kituo cha 4 cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh siku ya Jumapili, na kusababisha moto. Watu kumi na mmoja walijeruhiwa ambapo mtu mmoja aliawa mamlaka ya usafiri wa anga ya Saudi Arabia ilisema.
Vikosi vya muungano pia vilisema ulinzi wa anga wa Saudi Arabia ulinasa kombora la kitalii karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid.
πππππππππ
https://youtu.be/opy5HY-zp2U
1 hour ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
MELI NYINGINE YA MAFUTA YASHIKA MOTO, YAGONGA BOMU LA MAJINI HORMUZ
Meli ya tatu ya mafuta imeshika moto katika Mlango-Bahari wa Hormuz baada ya kugonga bomu la majini ilipokuwa ikijaribu kupita katika njia isiyoidhinishwa, Jeshi la Wanamaji la Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limetangaza.
Ofisi ya uhusiano wa umma ya Jeshi la Wanamaji la IRGC ilisema Jumapili usiku kwamba meli ya mafuta ya aina ya usafiri wa zamu, iliyokuwa imebeba mapipa 750,000 ya mafuta ghafi, ilijaribu kupita katika njia isiyoidhinishwa Jumapili alasiri, huku ikipuuza maonyo na tahadhari zilizotolewa na jeshi hilo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa meli hiyo iligonga bomu la majini, na kusababisha mlipuko pamoja na moto mkubwa.
Katika onyo jingine, Jeshi la Wanamaji la IRGC lilitangaza kwamba meli zote katika Mlango-Bahari wa Hormuz zitakazozima mifumo yake ya urambazaji na utambuzi zitachukuliwa kuwa ni za uhasama, na zitashughulikiwa kwa msimamo mkali na bila kusita.
Mapema Jumamosi, Jeshi la Wanamaji la IRGC liliripoti kwamba meli kubwa sana ya mafuta ilishika moto baada ya kugonga bomu la majini ilipokuwa ikijaribu kuondoka katika njia hiyo muhimu ya majini kupitia njia isiyoidhinishwa.
πππππππππ
https://youtu.be/B_Ifs4Y5ZYc
2 hours ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
UKRAINE YAISHAMBULIA TENA URUSI LICHA YA ONYO LA TRUMP.
Kampuni kubwa ya teknolojia ya Urusi, Yandex, imelazimika kusitisha shughuli zake katika kituo cha data kilicho karibu na Moscow baada ya kituo hicho kuharibiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine. Hili ni shambulio la tatu dhidi ya vituo vya Yandex ndani ya wiki hii.
Kampuni hiyo, ambayo imepewa jina la utani la βGoogle ya Urusi,β ilisema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kituo hicho kilichopo Vladimir, mashariki mwa mji mkuu Moscow, lakini baadhi ya huduma zake hazikupatikana kwa watumiaji.
Mapema wiki hii, Yandex ilisema ilikuwa ikikabiliwa na changamoto za kuendelea kutoa huduma zake baada ya vituo vyake viwili kati ya vitano vya data kushambuliwa na Ukraine.
Shambulio la Jumapili lilitokea saa chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuionya Ukraine kwamba inapaswa βkuacha kabisaβ kushambulia viwanda vya kusafisha mafuta vya Urusi.
πππππππππ
https://youtu.be/Qkjd9yLT4Pw
20 hours ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
WATU 109 WAFARIKI DUNIA BOTI IKIZAMA BAHARINI.
Wahamiaji wasiopungua 109, wakiwemo watoto 15, wamefariki dunia huku wengine 116 wakiripotiwa kupotea baada ya boti iliyokuwa imebeba watu 350 kuzama katika pwani ya Djibouti wakielekea Yemen, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limesema.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Oktoba 8 hadi 9 kaskazini mwa mji wa Obock, Djibouti, baada ya boti hiyo kupinduka ikiwa njiani kuvuka Mlango-Bahari wa Bab el-Mandeb kuelekea Yemen.
Kwa mujibu wa taarifa ya IOM iliyotolewa Jumapili, Oktoba 11, zaidi ya watu 80 walinusurika katika ajali hiyo. Wote walionusurika ni raia wa Ethiopia, ambao walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakisafiri kwa boti hiyo.
Miongoni mwa miili 109 iliyopatikana ni ya wanaume 52, wanawake 42 na watoto 15, wakiwemo wasichana tisa na wavulana sita. Timu za IOM zinafanya kazi pamoja na mamlaka za Djibouti kutoa msaada wa dharura kwa manusura.
πππππππ
https://youtu.be/5ZktScnrjCE
21 hours ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
MFUNGWA ALIYENUSURIKA MAJARIBIO MAWILI YA HUKUMU YA KIFO ATOKA HOSPITALINI.
Christa Pike, raia wa Marekani aliyenusurika jaribio la kunyongwa kwa sindano ya sumu, ameruhusiwa kutoka hospitalini na kurejeshwa gerezani siku 10 baada ya zoezi hilo lililofeli, kwa mujibu wa taarifa ya mawakili wake.
Pike, mwenye umri wa miaka 50, alidungwa sindano ya dawa ya pentobarbital mara mbili Septemba 30, katika jaribio la kutekeleza hukumu yake ya kifo katika jimbo la Tennessee. Zoezi hilo lilimuacha katika hali mahututi.
Mawakili wake wamesema Pike amerejea katika gereza alilokuwa akishikiliwa kwa takribani miaka 30 na ataendelea kupata huduma za matibabu. Hata hivyo, haijafahamika ni matibabu gani anayoendelea kupatiwa gerezani.
Pike alipata fahamu Jumanne na kuanza kuzungumza tena, jambo lililowashangaza wataalamu wa afya na mawakili wake. Wakili wake, Randy Spivey, amesema maneno yake ya kwanza yalikuwa, βNiko wapi?β na βWewe ni nani?β
πππππππππ
https://youtu.be/wtDIDub1QrE
23 hours ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
MASHAMBULIZI YA WAHOUTHI YATIKISA JUMUIA ZA KIMATAIFA, 12 WAUAWA UWANJA WA NDEGE, SAUDI ARABIA
Nchi mbalimbali pamoja na Umoja wa Mataifa zimelaani shambulizi la waasi wa Houthi nchini Yemen katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh, Saudi Arabia, lililosababisha vifo vya watu wasiopungua 12 na kujeruhi zaidi ya 300.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amelitaja shambulizi hilo kuwa baya sana, akisema nchi yake inatathmini uwezekano wa kujiunga na Saudi Arabia katika operesheni za kijeshi dhidi ya waasi hao.
Trump pia amesema anatarajia kuzungumza na kiongozi mkuu wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelilaani shambulizi hilo na kusema mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia yanakiuka sheria za kimataifa na yanapaswa kusitishwa mara moja.
Nchi nyingine zilizolaani shambulizi hilo ni pamoja na Misri, Qatar, Pakistan, Jordan, Oman, Palestina na Syria, huku zikionya kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu muhimu yanatishia amani na usalama wa eneo hilo.
Wakati hayo yakichomoza, Waasi wa Houthi wameonya matumizi ya viwanja vya ndege nchini Saudi Arabia
Msemaji wa waasi wa Houthi nchini Yemen, Yahya Saree, amezionya kampuni za usafirishaji wa mizigo baharini, mashirika ya ndege, wafanyakazi na wasafiri dhidi ya kutumia viwanja vya ndege na anga la Saudi Arabia, akisema maeneo hayo yako katika hatari ya kushambuliwa.
πππππππππ
https://youtu.be/0TwAuHrFFLo
23 hours ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
IRAN:HATUA DHIDI YA MELI ZINAZOKIUKA SHERIA HAZITAZUILIWA LANGO LA HORMUZ PEKEE
Iran imeonya kuwa operesheni dhidi ya meli zinazokiuka sheria haitajikita katika mlango bahari wa Hormuz pekee, ikisisitiza kuwa vyombo vitakavyotumia njia ambazo hazijadhinishwa vitafuatiliwa na kuchukuliwa hatua popote katika eneo hilo.
Katika taarifa, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji la Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesema meli yoyote itakayopita katika njia ambayo haijaidhinishwa na Iran itafuatiliwa na kuchukuliwa hatua bila kusita.
Iran inasisitiza kuwa meli zote zinapaswa kutumia njia maalumu za usafiri wa majini zilizowekwa ili kupitia mlango bahari wa Hormuz.
Kauli hiyo imekuja huku ripoti zikieleza kuwa baadhi ya meli za mizigo na meli za kubeba mafuta zimeanza kutumia njia mbadala zilizobuniwa katika wiki za karibuni ili kuepuka vikwazo vilivyowekwa na Tehran.
Wakati huo huo, Iran imesema haitafungua Lango la Hormuz kwa muda wote ambao inadai Marekani inaendelea na kile ilichokiita kizuizi cha majini dhidi yake.
πππππππππ
https://youtu.be/y3jQBXzLLvk
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
TRUMP ARUHUSU MAFUTA YA URUSI KUUZWA MAREKANI, ZELENSKY AKERWA
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amekosoa vikali tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu makubaliano ya kuingiza dizeli kutoka Urusi, akisema hatua hiyo ni sawa na kumpa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, "zawadi" inayochangia kuendeleza vita badala ya kuvikomesha.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Zelensky alisema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa Urusi kuimarisha uwezo wake wa kuendeleza vita dhidi ya Ukraine, akionya kuwa mapato yatokanayo na biashara hiyo yanaweza kufadhili mashambulizi zaidi.
Trump alitangaza kuwa Putin amekubali kusambaza tani 300,000 za dizeli mara moja kwa soko la Marekani na la kimataifa, zikifuatiwa na tani 500,000 mwezi Novemba na tani milioni moja zaidi baadaye.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Wizara ya Fedha ya Marekani itasitisha baadhi ya vikwazo dhidi ya usafirishaji wa dizeli ya Urusi hadi tarehe 7 Aprili, huku vikwazo vingine, ikiwemo mali za Urusi zilizozuiliwa katika benki za Marekani, vikisalia kutekelezwa.
ππππππππ
https://youtu.be/0kuEc6NnXQU
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
MAUAJI YA KIKATILI DODOMA, MUME AMUUA MKE, NA KWENDA KUNYWA POMBE NA KISHA KURUDI KULALA PEMBENI.
Taharuki imeibuka katika Mtaa wa Mailimbili Darajani jijini Dodoma baada ya mwanamume mmoja kudaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni, kabla ya kwenda kunywa pombe na kurejea kulala karibu na mwili wa marehemu.
Mwanamume huyo anayefahamika Kwa jina la Khatibu Mfaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39 anadaiwa kutekeleza tukio hilo dhidi ya mkewe Shukran Riziki mwenye umri wa miaka 30, katika tukio linalodaiwa kutokea oktoba 8 majira ya saa mbili usiku
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Kwa majirani wanandoa hao wamekuwa na historia ya kugombana mara kwa mara, huku mazingira ya tukio hilo yakiendelea kufuatiliwa na vyombo vya dola.
πππππππππ
https://youtu.be/_JJDfHtUjp0
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
#LIVE: MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFUGAJI TANZANIA ANAFUNGUKA MAZITO, βWANAPANGA ETI WANITEKEβ
πππππππ
https://youtu.be/f1Zs930Bu20
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Load more